WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE WASHAURIWA KUJIANDAA KUSTAAFU.
Akiendelea na ziara katika kata za: Chabutwa, Ipole na Ngoywa, Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu(W) Nico Kayange amewaasa watumishi wa Umma walio katika Wilaya hiyo kutumia vema nafasi za utumishi walizonazo kwa sasa ili waweze kujiandaa vema kustaafu wakiwa na uhakika wa kuishi maisha bora baada ya kustaafu nafasi hizo.
DHRO Kayange ameyasema hayo alipozungumza na watumishi wa Umma ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji (W) kuwatembelea watumishi wote wa Halmashauri ya Sikonge akisikiliza *kero* zao pamoja na kutoa maelekezo na maagizo ambayo watumishi wanapaswa kuyazingatia wanapotoa huduma bora kwa jamii."Fedha za kustaafu sio za kukopesha na kufanyia miradi mikubwa badala yake ni vema kuwekeza kwenye HISA ..kwa hiyo jiandaeni kustaafu vyema, Jiandaeni Kisaikolojia kuuacha Utumishi wa Umma...sio mstaafu unamkuta baada ya muda mfupi tu wa kustaafu anageuka ombaomba....ni kuaibisha utumishi wa Umma" DHRO Kayange.
Akijibu kero mbalimbali za watumishi ikiwemo upungufu wa watumishi, kufutiwa barua zao za kupandishwa vyeo kwa mwaka 2016 na 2021, baadhi ya watumishi kutotimiza wajibu wao, Mapunjo ya mishahara kutolipwa hadi sasa kero ambazo zimeanza kutatuliwa ikiwemo mapunjo ya Mishahara kuanzia Mwaka 2013 hadi 2020, DHRO Kayange amesema Serikali imetoa fedha zaidi ya Tsh.Milioni 500 kuwalipa mapunjo ya mishahara watumishi(659) wa kada mbalimbali na tayari wamelipwa.
Aidha DHRO Kayange ameongeza kuwa zaidi ya watumishi (865) mapunjo yao ya mishahara yamewasilishwa kwa Katibu - Mkuu - Utumishi kwa ajili ya kuchambuliwa ili fedha ikipatikana watumishi hao waweze kulipwa.
Katika hatua nyingine Kaimu Mkuu wa Idara ya Afya, Dkt.Grace Molel ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watumishi kuchanja chanjo ya UVIKO-19 kwa ajili ya kulinda afya zao na kuwalinda wengine ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya Ugonjwa huo.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa