WATAALAMU WA LISHE SIKONGE WASISITIZWA KUTOA ELIMU YA LISHE KWA WANANCHI.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amefungua kikao cha kamati ya lishe Wilaya ya Sikonge ambacho kinalenga kujadili mipango na mikakati mbalimbali ya utekelezaji wa majukumu ya kutoa huduma stahiki kwa jamii na kuhakikisha wananchi wanaishi maisha yenye Afya kwa kuzingatia lishe kamili.
Akifungua mkutano huo Mhe.Palingo amewasisiza wataalamu wa lishe na wadau mbalimbali kutoa Elimu wezeshi kwa wananchi juu ya umuhimu wa lishe kwa jamii huku akitoa maelekezo maelekezo kwa ofisi ya Mkurugenzi kusimamia na kuchangia endapo fedha itahitajika kutekeleza majukumu ya lishe."Badala ya kutia nguvu katika kutibu utapiamlo..tujikite katika kukinga utapiamlo kwa kuelimisha jamii zaidi juu ya lishe bora." DC Palingo.
Kwa upande wake Afisa Lishe Mkoa wa Tabora Bi Monica Yesaya amewataka watumishi na wataalamu wa afya kuwa mstari wa mbele kulinda afya zao kwa kuzingatia lishe ili wanapotoa Elimu kwa jamii wawe mfano wa kuigwa kwa kuwa na familia bora na zenye afya huku huku akisisitiza ushirikishwaji wa Sekta Binafsi.
Afisa Lishe Wilaya ya Sikonge Veronica Ferdinand amesema kikao hicho ni muhimu kwa kuwa kinakutana na wadau mbalimbali wa sekta binafsi na Serikali sambamba na wataalamu wa Afya kujadili mikakati na bajeti mahususi kwa ajili ya kuhakikisha Wilaya Sikonge inakuwa ni kitovu cha jamii yenye Afya Bora.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa