WANANCHI WAHIMIZWA KUBUNI MIRADI YA MAENDELEO.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amefanya ziara katika Kata ya Chabutwa na Kata ya Usunga tarehe 15/16 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea kata 20 za Wilaya ya Sikonge na kuwasisitiza wananchi kubuni miradi ya maendeleo ili kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili na si kusubiri Serikali ikiwa uwezo huo wanao.DC ameyasema hayo alipozungumza na wananchi katika vijiji mbalimbali vya kata hizo huku akihamasisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za Msingi zenye upungufu wa madarasa na kuongeza kuwa kazi ya kuleta maendeleo ni ya wananchi wote kwa kushirikiana na Serikali.Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Msingi Isack Thomas amewaasa wazazi kuwasimamia watoto wao vyema katika elimu kwa kuwa ni haki yao ya msingi kupata elimu bora.Akizungumza kwa niaba ya wananchi,diwani kata ya Chabutwa Mhe.Edward Almasi amempongeza DC Palingo kwa kufanya ziara na kusikiliza kero za wananchi hao na hatimaye kuzifanyia kazi,huku akiahidi kushirikiana nae katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Chabutwa.Kwa upande wake Diwani kata ya Usunga Mhe.Peter Kavishe amemhakikishia Mhe.Palingo kuwa atawashirikisha wananchi katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo hasa kampeni ya ujenzi wa madarasa.
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa