Na.Anna Kapama
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amekutana na Viongozi wa Chama Cha Ushirika Cha Wakulima (AMCOS) Kata ya Kiloli akiwahimiza hasa Viongozi kuwasimamia wakulima wa zao la Tumbaku kwa Msimu huu wa Mwaka 2022/2023 ili kuleta tija na kuwainua kiuchumi.
Mhe.Palingo ameyasema hayo kwenye kikao chake na wakulima na Viongozi wa Chama Cha Ushirika alipokutana nao kwa ajili ya kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili na kuwakemea baadhi ya wanachama wanaotaka Uongozi kwenye Chama Cha Ushirika pasipo kujihusisha na Kilimo hicho.
Katika hatua nyingine DC Palingo amewasisitiza wakulima kuondoa hofu kuhusu soko la Tumbaku kwani Serikali imelishughulikia.
"Tunakoelekea ni kuzuri zaidi, Makampuni ya kununua Tumbaku yanaongezeka, Serikali imeshulikia hilo, hakuna atakayeacha kuuza Tumbaku..hakutakuwa na ukomo kwa Mkulima ambapo ataruhusiwa kulima awezavyo" DC Palingo amefafanua.
Sambamba na hilo DC Palingo amewakemea Viongozi wa Vyama na Bodi za Ushirika kuwa waaminifu kwa kutojihusisha na Ubadhulifu badala yake waongoze vyama hivyo kwa kufuata taratibu na Sheria huku akimuagiza Afisa Ushirika kufuatilia kwa karibu ili wakulima wa Tumbaku wajikwamue kiuchumi.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa