Ndg. Riziki Kingwande Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania bara ametembelea Wilaya ya Sikonge na kuzindua shamba la mfano la alizeti la umoja wa wanawake wa CCM kata ya Tutuo. Akionge na umoja wa wanawake hao katika eneo la mradi ,Ndg Riziki aliwapongeza viongozi wa kata pamoja na kamati ya utekelezaji, kwa kumwalika kuja kuzindua na kuangalia mradi.Aliwasisitiza kuwa kupitia mradi huo baada ya kuvuna, waangalie namna ya kugawana ili kuwasilisha zile asilimia zetu kwa ngazi ya mkoa, wilaya na kata, na pia kuwawezesha wanawake wenye uhitaji bila kujali itikadi.
Pia Ndg Riziki amekemea vitendo viovu vya ukatili wa kijinsia kwa wototo hasa wa kike unaoendelea kufanyika katika jamii zetu zinazotuzunguka, hivyo amewaomba wazazi kusimamia malezi mazuri kwa watoto ili kuepukana na ukatili unaoendelea kufanyika. “Wazazi tuwe msitari wa mbele kupinga uonevu na kuhakikisha unaisha katika jamii zetu na kuondoa mila potofu na kuweka kipaumbele katika elimu ili watoto waweze kutimiza ndoto zao za kimsingi.”
Aidha Umoja wa Wanawake Sikonge umempongeza mgeni rasmi kwa kumzawadia gunia la mpunga, karanga na asali kama asante ya kuja kuzindua mradi wa shamba la alizeti na kuwashukuru viongozi wote walioambatana nae.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa