Timu ya wataalam kutoka ofisi ya Rais Tamisemi pamoja na timu ya wataalam kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Rais Tamisemi, Ndg. Joseph Mwacha, wametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Akizungumza na menejimenti ya halmashauri hiyo, Ndg. Mwacha amesisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu. Ameweka msisitizo kwenye falsafa ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inayotaka umoja wa kitaifa, maridhiano, mabadiliko, na ustahimilivu.
Aidha, Ndg. Mwacha amekabidhi Kanuni za uchaguzi wa viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa pamoja na mwongozo wa elimu ya mpiga kura kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Ndg. Selemani Pandawe.
Tangazo rasmi kuhusu uchaguzi huo lilitolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Mhe. Mohamed Mchengerwa, mnamo Agosti 29, 2024, likitangaza tarehe ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024.
Top of Form
Bottom of Form
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa