Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha ameyasema hayo leo Novemba 10,2023 katika kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha robo ya kwanza Julai hadi Septemba 2023/24 katika Ukumbi wa Hospitali ya Wilaya ya Sikonge.
Akifungua kikao hicho Mhe. Chacha amesisitiza kufanya kazi kwa bidi na weledi ili kufikia malengo ya serikali ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
Aidha wakiwasilisha Taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Idara ya Afya ya Msingi pamoja na mazingira wataalamu toka vitengo mbalimbali vya afya wameeleza jinsi shughuli hizo zinavyotekelezwa ikiwemo Idara ya Chanjo,Lishe na Afya ya Uzazi .
Taarifa imeonesha kuongezeka kwa idadi ya akinamama wajawazito wanaojifungua katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na mwitikio mkubwa wa wananchi katika kupata chanjo mbalimbali kama vile surua,polio pamoja na chanjo mpya ya saratani ya shingo ya kizazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Christopher Nyalu amemshukuru Mhe. Chacha na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote yaliyoshauriwa na wajumbe wa kikao.
Akifunga kikao hicho Mhe. DC amesisitiza upandaji wa miti ya matunda hususani miche ya Miembe katika maeneo ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC), eneo la Kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki pamoja na Barabara ya bomani.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa