Mwenyekiti wa Halmashauri yaWilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope ameongoza baraza la madiwani la kufungamwaka, ambapo baraza hilo limepokea na kujadili taarifa za utendaji nauwajibikaji wa shughuli za maendeleo za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Katika baraza hilo, madiwaniwamepata nafasi ya kushiriki katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti waHalmashauri. Kwa umoja, baraza limemchagua Mhe. Gasto Andrea Lwambano, diwaniwa kata ya Kiloleli, kuendelea na wadhifa huo kwa kupata kura zote za ndio 26.
Aidha, baraza limepitishauteuzi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Halmashauri watakaohudumu kwa kipindicha mwaka mmoja, na pia limepitisha ratiba ya vikao vya Halmashauri.
Akizungumza katika barazahilo, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Mhe. Cornel Lucas Magembe, amesisitiza umuhimuwa ushiriki wa viongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Mhe. Magembe ametoawito kwa viongozi kuelimisha umma na kuhamasisha jamii kushiriki katikauchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024, kwa ajili ya kuchaguaau kuchaguliwa kuwa viongozi.
Akifunga baraza hilo Mhe. Magopeamewashukuru waheshimiwa madiwani kwa moyo wao wa kujitoa kuwahudumia wananchiwa Sikonge bila kuchoka na amewasihi kuendelea kuchapa kazi ili kuwaleteamaendeleo wananchi waliowachagua.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa