TFS WAHIMIZA WANANCHI KUTUNZA MISITU.
Na.Anna Kapama.Wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS) wamewataka wananchi Wilayani Sikonge kuitunza misitu hasa wakati huu wa kiangazi baada ya kutembelea katika misitu mbalimbali iliyopo Wilayani hapo na kujionea uchomaji moto holela wa misitu.
Kwa upande wake Kamanda mhifadhi kanda ya Magharibi (TFS) Ebrantino Mgie ,amesema uchomaji wa misitu una athari nyingi si tu kwa binadamu bali wanyama wanaoishi katika misitu hiyo wanaathirika kwa kufa,na wengine kukimbia makazi yao kutokana kadhia hiyo.Aidha,Kamanda Mgie amewataka wananchi kuacha vitendo hivyo na endapo wataona kuna moto katika msitu washirikiane kuuzima ili kunusuru maisha ya viumbe hai na kutunza mazingira.
https://web.facebook.com/100024087722562/videos/pcb.1033008044178777/262505365730854
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa