Na.Anna Kapama_Sikonge_Tabora
Meneja wa TARURA Wilaya ya Sikonge Mhandisi Eligdius Method amesema katika Mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga fedha Tsh.Bilioni 2.45 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Mtandao wa Barabara za Wilaya ya Sikonge na kuongeza kuwa TARURA Wilaya ya Sikonge imedhamiria kufanya matengenezo ya Barabara zote kabla ya Msimu wa Mvua .
Mhandisi Method ameyasema hayo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa robo ya Nne 2021/2022 uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri .
Aidha, Mhandisi Method amewataka Madiwani kutoa Ushirikiano kwa wakandarasi wanapokuwa wakitengeneza barabara katika maeneo yao ikiwemo kuhamasisha wananchi waweze kuomba ajira zinazotolewa na wakandarasi.
"Vijana wa Wilaya ya Sikonge wanatakiwa kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na wakandarasi wakati wa Ujenzi wa Barabara, moja ya maelekezo ya miradi hii ni kuwanufaisha wahusika wa maeneo hayo, wanaposhirikishwa katika Ujenzi wa Barabara wataona umuhimu wake na namna ya kuitunza Barabara" Mhandisi Method
Katika hatua nyingine Mhandisi Method amewasisitiza wananchi kutoa taarifa za uharibifu wa Barabara kwa kupiga namba *152*00# Kisha kufuata maelezo mengine ili kutoa taarifa za uharibi wa uliosababishwa na Barabara kujifunga, ajali, Miti kuanguka Barabarani, Daraja kubomoka ambapo taarifa hizi zitapelekwa kwa mamlaka na kufanyiwa kazi, na mtoa taarifa atapewa mrejesho wa utatuzi wa changamoto hiyo.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa