Wataalam wa maswala ya Lishe wamefika Leo Sikonge na kukutana na Kamati ya lishe Wilaya, ambayo Mwenyekiti wake ni Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, Bi. Martha Luleka. Wataalam hao ambao wametoka ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi Marium Mwita na Bwa. Apolinary Seiya wametoa mada mbalimbali zinazohusu lishe na namna ya kuelimisha jamii.
Aidha, wataalam hao wamesisitiza kutenga bajeti ya lishe itakayotekeleza shughuli za lishe ikiwemo kampeni ya Kitaifa ya utoaji matone ya vitamini A na uhamasishaji wa akina mama kutumia dawa za kuongeza damu wakati wa ujauzito.
Nae Mkuu wa Wilaya Sikonge, Peres Magiri ambae alikuwa mgeni rasmi ameitaka Kamati ya lishe Wilaya kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwa sababu lishe ni jambo muhimu sana katika ukuwaji wa watoto ambao baadae ndio viongozi wa taifa.
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mhe. Peter Nzalalila amtaka Afisa Lishe Wilaya, Mario Sibamenya pamoja na Kaimu Maganga Mkuu Wilaya kuhakikisha taarifa za maswala ya lishe na utekelezaji wake kupitishwa katika vikao vya Kamati za kudumu za Halmashauri hasa Kamati ya elimu, afya na maji ili kujenga uelewa wa pamoja na kusaidiana katika kuelimisha jamii.
Kabla ya kikao kuisha Mkurugenzi mtendaji, Mkuu wa Wilaya pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri waliondoka kuelekea Mkoani kuhudhuria kikao cha maandalizi ya jukwaa la viwanda pia kusaini mkataba juu ya maswala ya lishe.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa