SIKONGE YAFANYA MKUTANO WA MAOMBI NA MAOMBOLEZO YA HAYATI MHE.DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.
Na.Anna Kapama-Sikongedc
Viongozi wa madhebu ya kidini, Wakuu wa Taasisi, watumishi wa umma na wananchi wa Wilaya ya Sikonge Leo tarehe 23/3/2021 wamefanya Ibaada maalumu ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt.John Pombe Magufuli aliyefariki tarehe 17 Machi, 2021.
Akitoa hotuba fupi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Anna Chambala amewataka wananchi kuendelea kuyaishi kwa vitendo maono ya Hayati Dkt John Pombe Magufuli kwa kudumisha amani,upendo na mshikamano huku wakimtanguliza Mungu kwa kila jambo.
Aidha, amesikitishwa na kulaani vikali vitendo vya watu wachache wasioitakia mema Nchi ya Tanzania kwa kuonesha kufurahishwa na kifo cha shujaa huyu wa taifa la Tanzani na kuwataka waache maramoja.
Hafla hiyo ya kumuombea imefanyika katika viwanja vya CCM Wilaya ya sikonge na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi waliojaa majonzi na huzuni ya kumpoteza kiongozi shujaa wa Tanzania.
Nae Sheikh wa Wilaya ya Sikonge,Jumanne Hassani amewataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu ambacho Taifa linapitia na kumuombea ili wanaobaki waweze kuenzi yaliyoachwa na Hayati dkt John Magufuli.
Aidha, Katibu Tawala wa Wilaya ya Sikonge, Renatus Mahimbali akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kukumbuka maendeleo yaliyofanywa na Hayati dkt John Magufuli ikiwemo miundombinu bora ya barabara,umeme na maji, miradi ambayo imetekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wake huku akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MHE.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ni kiongozi anaeaminiwa na kwamba atasimamia maono na dira ya Taifa.
Kwa upande wake wakili Paroko wa kanisa Katoliki, Fr. Deo Shiwala,akieleza mambo makubwa ambayo ameyafanya ikiwemo miradi ya maendeleo na huduma bora za jamii zinazopatikana Wilaya ya Sikonge ni kumbukumbu tosha kuonesha namna ambavyo Hayati Dkt John Magufuli alivyojitoa kwa kuwatumikia watanzania.
Ibaada hiyo ya maombi maalumu imehudhuriwa na viongozi wa madhebu mbalimbali ya kidini,viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) akiwemo mwenyekiti wa chama hicho Anna Chambala,Watumishi wa Umma Wilaya ya Sikonge,Vyombo vya ulinzi na usalama na mamia ya wakazi wa Sikonge.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa