SIKONGE-SERIKALI YAUPANDISHA HADHI MSITU WA ITULU HILL
NA Evelina Odemba
SERIKALI yaupandisha hadhi Msitu wa Itulu Hill kuwa Msitu Asilia,ikiwa ni miongoni mwa Misitu michache ya asili inayopatikana Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa wakala wa misitu Tanzania (TFS) kanda Valentine Msusa alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Kipili iliyoko wilayani Sikonge Tabora eneo ambalo msitu huo unapatikana na kuwataka kujivunia hatua hiyo kwani mbali na kuwa na manufaa makubwa kwa serikali, jamii itanufaika pia.
Alibainisha kuwa lengo la serikali ni kuendeleza maliasili zilizopo na kuzihifadhi ili zinufaishe kizazi kilichopo na kijacho akitolea mfano Mti jamii ya mninga ambao umekuwa kwenye hatari ya kutoweka kwa sababu ya kuvunwa sana hivyo uwepo wa msitu huo utasaidia kuuifashi.
“hatuko tayari kupoteza Tembo wetu, hatuko tayari kupoteza miti asilia, hivyo basi yeyote atakayekiuka agizo la serikali la kuhuifadhi Msitu huu, hatutomvumilia, tutabanana nae huko huko ndani kwa ndani” alisema.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Mhe. Musalika Makungu ambaye amekuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira kwa kuwataka wananchi kueshimu agizo la serikali kwa kuwa walinzi wa msitu huo huku akiwataka kutoa taarifa kwa viongozi usika mara wanapoona kundi la watu wakishiriki uharibifu wa Msitu huo.
Sambamba na hayo aliwataka wananchi kuitumia fulsa hiyo kwa kusoma masomo ya utalii kwani Msitu huo unategemewa kutumika kwa shuguli za utalii na tafiti mbalimbali. Hivyo kuwa na elimu ya utalii kwa wanajamii kutawapatia ajira itakayokuza kipato chao.
Wananchi wa Kipili wakipokea maelekezo toka kwa Mkuu wa Wilaya. Mhe. Peres Magiri aliyesimama katikati.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri alipokea maelekezo hayo kwa kusema kuwa akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya atahakikisha Msitu huo unalindwa vyema, na yeyote atakayekutwa akifanya shuguli yeyote ndani ya Msitu huo bila kibali atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini. Sanjari na hayo aliishukuru serikali kwa kuupandisha msitu huo hadhi na kusema ni jambo la kujivunia kwa wana Sikonge wote.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa