SERIKALI YAONYA WAFUGAJI WANAOVAMIA MISITU YA HIFADHI.
Na Evelina Odemba
SERIKALI yapiga marufu wakulima na wafugaji kuvamia eneo la Misitu ya hifadhi na kufanya shuguli zao kwenye misitu hiyo.
Hayo yalibainishwa na ,Meneja wa kanda wa wakala wa misitu (TFS) bwana Valentine Msusa alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Kipili iliyopo Wilayani Sikonge katika mkutano wa hadhara uliohuzuliwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, kamanda wa Polisi Mkoa, na Mkuu wa Wilya ya Sikonge aliyekuwa mwenyeji wa mkutano huo.
Aidha bwana Msusa alionya wafugaji wote wanaovamia maeneo ya hifadhi na kujimilikisha maeneo hayo kinyume cha utaratibu uliowekwa kuwa watapigwa faini huku akiweka bayana kuwa kfugaji atakayekutwa na mifugo yake ndani ya hifadhi atakuwa amevunja makosa matatu kwa pamoja hivyo atatozwa faini isiyopungua laki tatu mpaka milioni tisa kwa makosa hayo.
Hata kivyo katibu Tawala wa Mkoa Mhe. Musalika Makungu alisema kuwa lengo la serikali sio kutoza faini bali kuhakikisha taratibu zilizowekwa zinafuatwa huku akongeza kuwa serikali inawatambua wafugaji kama sekta muhimu inayochangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi. Hivyo basi kwa thamani hiyo Wilayani Sikonge kumetengwa eneo maalum litakalokodishwa kwa wafugaji kwa shuguli za malisho huku akiitaja sehemu ya hifadhi ya Ipembampanzi kutengwa kwa shuguli hiyo.
“sio jambo la kufurahisha kuwa mfugaji anayepigwa faini mara kwa mara, mimi mwenyewe ni mfugaji wa siku nyingi ninayefuga kwa kufuata utaratibu”, alisema na kuongeza kuwa wakati wa kufuga mifugo mingi umepitwa na wakati na kuwataka wafugaji kwenda na wakati wa kufuga mifugo michache watakayoweza kuihudumia kwa malisho.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri akizungumza na wananchi wa kata ya Kipili alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara.
Aliyasema hayo alipokuwa akijibu swali la mfugaji Didia Mapowogo aliyetaka kujua lengo la serikali kuhusu kuongeza eneo la kuchungia kwani eneo lililotengwa ni dogo kulinganisha na idadi ya mifugo inayopatikana eneo la Kipili pekee.
Naye Mkuu wa Wilaya Mhe. Peres Magiri aliwataka wananchi wilayani kwake kutii sheria bila shuruti. Huku akifafanua kwa wakulima ambao mazao yao yapo katika maeneo ya hifadhi kujiandikisha kwa uongozi wa kata ili wapewe muda wa kuyavuna na kusisitiza kuwa baada ya kuvuna hakuna mkulima au mfugaji atakayeruhusiwa kuingia kwenye maeneo ya hifadhi bila kibali.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa