TABORA
Na.Anna Kapama
Utalii umefanyika katika maeneo mbalimbali ya Vivutio na ya kihistoria Mkoa wa Tabora ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Balozi.Dkt. Batilda Buriani na watalii wengine wamefika katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Tabora(TABORA BOYS) ambapo Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu J.K Nyerere alisoma hapo na kuoneshwa ramani ya Tanzania na maeneo ambayo Baba wa Taifa hili alifika.
Aidha,Balozi Batilda na watalii wengine wamefika katika Chuo Cha Nyuki na kujionea Jinsi ya Ufugaji wa Nyuki Mchakato wa usindikaji wa Mazao ya Nyuki, pamoja na kutembelea katika bustani ya wanyama Pori ya Tabora(Tabora zoo) , Tembe la Ukumbusho wa Dr Livingston ambapo maeneo yote hayo watalii wameweza kupata Elimu ya kutosha pamoja na kuangalia Vivutio vilivyopo.
Katika Mnara wa kumbukumbu ya uamuzi wa Busara(Azimio la Tabora) wa Mwaka 1958 uliofanyika Mjini Tabora ambao ulikuwa ni Uchaguzi wa kwanza na kura tatu zilipigwa yaani wazungu, waarabu na Waafrika ,mahali ambapo Mwalimu J.K.Nyerere alihutubia wananchi katika Soko kuu la Tabora Mjini kwa hisia na kuangua kilio akiwaeleza madhila ya Ukoloni ambapo Chama Cha TANU kilishinda viti 28 kati 30 na wagombea wa TANU walishinda dhidi ya wapinzani wa UTP na ANC.
Aidha,baada ya utalii wa Mjini Tabora Msafara wa watalii utaelekea katika Uwanja wa Kolimba Wilayani Kaliua ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tabora ataitambulisha Filamu iitwayo THE ROYAL TOUR iliyochezwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kisha kutazamwa na Wananchi wote.
#theroyaltour
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa