Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Utumishi Bi. Elizabeth Makyao akiambatana na Wawezeshaji toka ofisi ya Rais Utumishi wameendesha mafunzo ya mifumo mipya ya Pepmis na Pipmis kwa Wakuu wa Idara na Divisheni katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Akiwasilisha mada Bwana Aidan Lucas Mwezeshaji toka Ofisi ya Rais Utumishi amesema zoezi hili linaendeshwa nchi nzima na lengo kubwa ni kuhama katika mifumo ya kizamani ya upimaji wa utendaji kazi wa watumishi ya kutumia karatasi kama vile Confidential Appraisal System ambayo ilitumika toka mwaka 1961 hadi 2004. Open Performance Review Appraisal System (OPRAS) iliyotumika toka mwaka 2004 hadi 2013 na Kwenda katika mifumo mipya ya Pepmis na Pipmis ambayo itaanza kufanya kazi ifikapo tarehe 1 Januari 2024.
Mafunzo haya yatafanyika kwa siku tatu wilayani Sikonge na yanaendeshwa nchi nzima mpaka kufikia tamati Disemba 31, 2023.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa