_Awaasa wananchi kutunza Barabara
_Ameahidi kukarabati Madaraja yaliyoharibiwa na Mvua.
Sikonge_Tabora
Meneja wa TARURA Mkoa wa Tabora Mhandisi Edward Lemelo ametembelea kata kilumbi na Kipili kuona uharibifu wa mvua, iliyoharibu madaraja ya Kilumbi na Kipili na kujadili namna yakurudisha mawasiliano.
Aidha, Meneja wa TARURA Wilaya ya Sikonge Mhandisi Elgidius Method amebainisha kuwa
Pamoja na sababu zingine za zilizosababisha uharibifu ikiwemo kukatika Kwa miti na kusombwa na Maji Hadi kwenye Madaraja hayo amezitaja pia uharibifu unaochangiwa na baadhi ya wananchi wanaofanya Shughuli za Kilimo Kwa kuchimba majaruba ya kuchepusha Maji karibu na Barabara na kuwataka kuacha maramoja.
Katika Ziara hiyo Mhandisi Edward Lemelo amewataka wananchi kuacha maramoja kuhamisha Maji Kwa kuchimba majaruba Kwa ajili ya Kilimo katika maeneo ya Barabara
na kuahidi kutenga bajeti Kwa ajili ya kufanya marekebisho ya Madaraja hayo ili kurejesha Mawasiliano Kwa wananchi wa kata hizo.
Katika Ziara hiyo Maneja wa TARURA Mkoa wa Tabora aliambatana na Meneja wa TARURA Wilaya ya Sikonge pamoja na Watendaji wa Kata na wenyeviti wa vijiji.
#kaziiendele
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa