MAKARANI WATAKIWA KUZINGATIA MAELEKEZO ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA SENSA.
Na.Anna Kapama
16 Agosti, 2022
Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Wilaya ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amewasisita Makarani wa Sensa kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa na wakufunzi wa Sensa ili kufanikisha zoezi Hilo linalotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022 .
Mhe.Palingo ameyasema hayo Leo wakati akifunga Mafunzo ya awamu ya kwanza kwa Makarani wa Sensa ambao wanatarajia kufanya kazi hiyo Usiku wa kuamkia Agosti 23, 2022 na kuwataka kufanya zoezi Hilo kwa uadilifu na Uzalendo ili Idadi ya wakazi wa Sikonge iendane na Mipango ya Maendeleo inayopangwa na Serikali.
"Naamini tutaenda kufanya kazi vizuri na kwamba zoezi hili tutalifanikisha..na Wilaya yetu iwe kati ya Wilaya zilizofanya vizuri katika Zoezi hili la Sensa" Mhe.Palingo
Katika hatua nyingine Mratibu wa Sensa Wilaya ya Sikonge Aidan Frument amesema mafunzo yamefanyika vizuri , na kuwataka makarani kutunza Vifaa vyote vitakavyotumika katika kuhesabu watu ikiwemo Vishikwambi.
#sensakwamaendeleoyetu
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa