Maadhimisho ya upandaji miti Duniani, Wilaya ya Sikonge imeadhimisha siku hii kwa kupanda miti katika maeneo ya TASAF, Barabara kuu, Barabara ya Dear mama na Barabara ya kuelekea TAKUKURU. Mgeni rasmi akiwa Mku wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peresi Magiri amesisitiza usimamizi na ufuatiliaji wa miti iliyopandwa ndani ya Wilaya ili isikauke kwa jua na isiharibiwe na mifugo. Aidha, amezitaka taasisi kama vile shule na Halmashauri kuwa na vitalu vya miti ili kurahisisha upatikanaji wa miche.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa