KUELEKEA SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI TAREHE 28.10.2022
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe anawaalika wananchi wote wa Wilaya ya Sikonge kuhudhuria katika Maadhimisho ya Kichaa Cha Mbwa ambayo yatafanyika katika Uwanja wa Soko la TASAF Kata ya Tutuo Kuanzia saa 1:30 Asubuhi.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo ambaye atahutubia wananchi sambamba na wageni mbalimbali watakuwepo.
Aidha, Wananchi wenye mbwa wanahimizwa kuwaleta katika Viwanja hivyo ili patiwe chanjo ya Kichaa Cha Mbwa BURE.
KAULI MBIU KWA MWAKA 2022: KICHAA CHA MBWA, AFYA MOJA, VIFO SIFURI.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa