Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Cornel Lucas Magembe ameongoza hafla fupi ya kukabidhi madawati mapya 56 kwa shule ya msingi Majengo yaliyotengenezwa kwa fedha toka mfuko wa jimbo.
Akisoma taarifa ya mradi huo wa utengenezaji wa madawati hayo 56 Bw.Aidan Frument,Mkuu wa divisheni ya Mipango na Uratibu amesema Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ina jumla ya shule za msingi 109 zenye wanafunzi 73,676 kati yao wavulana wakiwa ni 36,514 na wasichana 37,162 amabapo mahitaji ya madawati ni 19,513 na yaliyopo ni 14,403 hivyokufanya kuwa na upungufu wa madawati 5,110.
Bwana Frument ameongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imetenga jumla ya shilingi milioni 60 kwa ajili ya kutengeneza madawati 833.
Akipokea taarifa hiyo Mhe. Magembe amempongeza mbunge wa jimbo la Sikonge Mhe. Joseph Kakunda kwa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Sikonge kwa uadilifu mkubwa kwa kuhakikisha fedha za mfuko wa jimbo zinatumika ipasavyo kutatua kero mbalimbali jimboni kwani kwa mwaka wa fedha 2023/2024 zaidi ya shilingi milioni 102 zimetumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo la Sikonge.
Mhe. Magembe ameendelea kusisitiza wananchi kuzingatia maagizo ya Serikali hususani suala zima la lishe shuleni,kwa kuhimiza wananchi kulipa kipaumbele suala la kuchangia chakula shuleni ili watoto waweze kupata afya na utulivu wakati wa masomo. “Watoto wakipata chakula shuleni;wataweza kubaki shuleni lakini watapata utulivu na kuchochea uelewa darasani” amesema Mhe. Magembe.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Mhe. Rashid Magope ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge,Ndg. Seleman Pandawe,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge,Bw. Maulid Ally,Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Sikonge,Bi. Faraja Hebel kwa niaba ya Katibu Tawala wa Wilaya,Mhe. Peter Nzalalila,Diwani wa kata ya Sikonge pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa