Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa hatua za haraka walizozichukua katika tukio la tuhuma za ubakaji lililotokea Hospitali ya Wilaya ya Sikonge.
Pia Watumishi wa Afya wamesaini Mikataba ya uhadirifu ya utendaji kazi ili kuweza kukumbuka wajibu wake wa kazi kwa kufata sheria, kanuni, misingi na miongozo. Sekta ya Afya zinatutaka kuzingatia utu, tuwe na dhamira safi, tujali masirahi ya Umma na tuwajali wagonjwa nakutumia lugha safi na tutoe huduma safi inayozingatia Maadili ya sekta ya Afya.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha ameongea na watumishi wa Idara ya Afya amesisitiza sana juu ya Maadili ya utumishi na kuwataka watumishi kuzingatia viapo walivyo hapa vya semina ya siku moja ya maadili ya utumishi wa umma.
Aidha Mboya ameagiza kwa watumishi wa Afya kuwa wanategemea nidhamu na uhadirifu katika maeneo ya kazi na nje ya kazi hili ni pamoja na kuacha ulevi kazini na kuacha kufanya vitendo viovu kwa wagonjwa. Ukibainika umefanya tukio hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa. Pia Chacha amempongeza Mganga Mkuu wa Wilaya Dr Christopher Nyalu kwa kuwa mchapakazi na mwadilifu na aendelee kuwa mfatiliaji wa kila mtumishi wa Idara ya Afya na kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma iliyo Bora.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa