Na.Anna Kapama
Sikonge_Tabora
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango imeendelea na ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo ambapo katika Shule ya Sekondari Msuva Kamati imekagua ukarabati wa Maabara ya Fizikia na iliyogharimu Tsh.Milioni 30 na kuwapongeza kwa ujenzi wenye Ubora pamoja na kubakiza fedha.
"niwapongeze wameweza kuheshimu fedha za Serikali baada ya matumizi na imebaki Milioni 2.3 , nawashauri waendelee na uadilifu huu katika miradi mingine" Mhe.Mayeka Mbussa, Diwani Kata ya Kilumbi
"Mimi niwapongeze kwa jinsi ambavyo wamejipanga, Ofisi ya Mkurugenzi anamaelekezo mazuri..mradi kama huu ukiona uko hivi ni juhudi ya Mkurugenzi na wataalamu..Maneno yangu ni kupongeza mradi ni mzuri" Mhe.Sada Sizya, Diwani Kata ya Igigwa
"Sio dhambi sana kupongeza sehemu ukikuta wamefanya vizuri, Msuva Sekondari wamejitahidi Kazi ni Nzuri, tumeona na Chenchi ipo.."Mhe.Gastor Lwambano, Diwani Kata ya Kiloleli
Shule ya Sekondari Msuva ilipokea Fedha kiasi Cha Shilingi Milioni 30 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ukarabati wa Chumba Cha Maabara ya Fizikia hata hivyo wametumia milioni 27.7 kukamilisha na fedha ikiwa imebaki Tsh.Milionin 2.3
Ziara inaendelea....
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa