KAFUM YAIKAGUA KAMAGI
KAMATI ya Fedha, Uongozi na Mipango (KAFUM) ilitembelea shule ya Sekondari Kamagi ili kujionea namna mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa, bwalo la chakula pamoja na bweni la wanafunzi unavyoendelea.
Ikiwa shuleni hapo kamati hiyo ilifanikiwa kukutana na uongozi wa shule pamoja na wanakamati wa ujenzi ambapo walielezea shuguli mbalimbali zinazohusu ujenzi,gharama na ununuzi wa vifaa huku wakiitaja changamoto ya fedha kuonekana kutotosha kuukamilisha mradi huo.
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango pamoja na walimu na wajunbe kamati ya Ujenzi wakizungumza na wanafunzi shule ya sekondari Kamagi walipotembele shuleni hapo.
Akijibu hoja hizo mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Peter Nzalalila ambaye pia ni mwenyeketi wa kamati ya Fedha, alitoa ushauri kwa wajumbe wa kamati ya ujenzi kuhakikisha wanawasimamia mafundi vizuri ili kazi ifanyike kwa uharaka na ubora unaotakiwa huku akikemea kisingizio cha pesa kutotosha. Akitolea mfano wa Wilaya ya Nzega ambayo imefanikiwa kumaliza mradi unaofanana na huo mapema kwa fedha zilezile zilizotolewa kwenye mradi wa Kamagi hivyo kuitaka Sikonge ifuate nyayo hizo.
Miongoni mwa wajumbe waliochangia ni diwani wa kata ya Kipili Mhe. Maria Ngido aliyesema kuwa ni vyema pia ujenzi huo ukabana matumizi kwa kuongeza jengo la ofisi ya walimu kwa pesa hizo zilizotolewa, huku akiitaja njia mojawapo ya kubana matumizi ni kushirikisha wananchi katika kujitolea kwani miradi hiyo imeletwa kwa ajili ya wananchi wa eneo hilo.
Akiongezea swala la kujitolea Mhe. Nzalalila alisema kuwa ni wakati sasa wa kutumia Skauti, Mgambo, pamoja Timu ya mpira wa mguu kujitolea katika ujenzi huo ambapo aliishauri kamati kuwapangia siku maalumu ya wao kushiri kwani uwepo wao katika jamii una mchango mkubwa ikiwemo kushiriki katika shuguli za maendeleo ikiwemo ujenzi unaoendelea Kamagi.
Shule ya sekondari Kamagi ilipata shilingi milioni 316,600,000 ikiwa ni fedha kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula, vyumba vitatu vya madarasa, mabweni ya wanafunzi pamoja na matundu sita ya vyoo, hadi KAFUM inafika shuleni hapo ujenzi bado unaendelea ambapo mwenyekiti wa kamati ya ujenzi alisema kuwa wanatarajia kukamilisha baada ya siku 90 tokea fundi akabidhiwe mkataba wa ujenzi.
Mbali na kukagua miradi hiyo kamati pia ilishiriki kumwaga zege kwa kubeba kokoto ikiwa ni njia ya kuhamasisha wananchi wajitolee kwenye shughuli za maendeleo. Vile vile walizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kamagi ambapo walitoa ushauri kwa wanafunzi hao juu ya kuzingatia elimu wanayopewa kwa kuweka malengo katika masomo yao.
Mwenyekiti KAFUMU mwenye shati ya mistari Mhe. peter Nzalalila na wajumbe wakijitolea Kamagi Sekondari.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA TEKINOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA)
SIKONGE.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa