Sikonge_Tabora
24. 10.2022
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango(KAFUM) Wilaya ya Sikonge inafanya ziara ya Siku mbili ikikagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa lengo la kujua thamani ya fedha na Ubora unaotumika katika kutekeleza Miradi hiyo.
Kamati hiyo itakagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Sekta ya Afya na Elimu.
Aidha, Kamati hiyo inayo ongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Rashid Magope sambamba na Katibu wa Kamati ambae ni Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Seleman Pandawe imeundwa na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa