• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Sikonge District Council
Sikonge District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Idadi ya Watu
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Mifugo na uvuvi
      • Afya na Ustawi wa jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mazingira na Taka ngumu
      • Kilimo, Umwagilaji na Ushirika
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Uchimbaji wa Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo Ndogo
    • Miongozo Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya sanaa
      • Sanaa za picha
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba
    • Habari mpya
    • Matukio

HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE YAADHIMISHA MIAKA 61 YA MUUNGANO KWA KUFANYA USAFI

Imewekwa: April 26th, 2025

Na Edigar Nkilabo

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wilayani Sikonge kumekuwa na shamrashamra mbalimbali ikiwemo kushiriki katika zoezi la usafi na utunzaji wa mazingira ambapo viongozi wa wilaya, watumishi na wananchi wameungana kufanya usafi katika mitaro ya Barabara za mitaa pamoja na maeneo ya soko la Kariakoo na TASAF.

Akiongoza zoezi hilo Katibu Tawala wa Wilaya ya Sikonge Ndg.Andrea Ngh’wani  amesema kuungana na kufanya usafi imekuwa njia nzuri ya kuusherehekea muungano wetu pia ni ishara njema ya umoja wetu hivyo tuungane na serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na kujenga utamaduni wa kufanya usafi na kutunza mazingira ya umma na yale yanayotuzunguka ili kuwa salama dhidi ya magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na uchafu.

“Zoezi hili la kukutana na kufanya usafi ni ishara ya kuudumisha muungano wetu na jamii ilifanye zoezi hili la usafi kuwa endelevu ili mazingira yawe safi na salama na hapo tutakuwa mbali na magonjwa ya mlipuko” amesema .

Aidha Katibu Tawala amewataka wananchi wa Sikonge kujitokeza kwa wingi kesho tarehe 26/04/2025 kwenye kilele cha sherehe ya miaka 61 ya Muungano, ambazo zitafanyika katika Uwanja wa TASAF kwa kunogeshwa na Bonanza la michezo ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba na kufukuza kuku.

Kwaupande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Nico Kayange amesema kazi iliyofanyika leo ya usafi ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 61 ya Muungano wetu ambao ni tunu na inaacha alama kwa wakazi wa Sikonge ambao wanapaswa kuendeleza zoezi hili hata siku zingine ambazo si za sherehe.

Zoezi la usafi na utunzaji wa mazingira limehusisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wilya ya Sikonge, Viongozi na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Watumishi, wananchi pamoja na Wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Sikonge (FDC).

Matangazo

  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUKODISHA CANTEEN [MGAHAWA] MPYA KWENYE JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZAABUNI YA KUMPATA MWEKEZAJI KATIKA KIWANDA CHA KATI CHA KUCHAKATA MAZAO YA NYUKI(MARUDIO) June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA USAFI KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA ULINZI June 07, 2023
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA SIKONGE YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOPENDEKEZWA KUPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    May 13, 2025
  • UZINDUZI WA SHULE YA MSINGI KININGA - KATA YA IPOLE

    May 09, 2025
  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA WILAYANI SIKONGE

    May 07, 2025
  • KIKAO CHA TATHIMINI YA MKATABA WA LISHE WILAYANI SIKONGE

    April 29, 2025
  • Angalia zaidi

Video

Ziara ya Waheshimiwa Madiwani Wilayani Rungwe - Mbeya.
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Zabuni
  • Matukio
  • Matangazo
  • Habari

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Mkoa wa Tabora
  • TAMISEMI
  • Urambo DC
  • UTUMISHI
  • Kaliua DC

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC

    Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora

    Simu: 0767135460

    Simu: 0767135460

    Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma zetu

Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa