"FEDHA ZA MAENDELEO ZITUMIKE KAMA INAVYOTAKIWA" MJUMBE KAMATI KUU CCM TAIFA AFADHAL T.AFADHAL
Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Ndg.Afadhal T.Afadhal amewasisitiza viongozi wa Chama cha Mapinduzi na watendaji wa Halmashauri hiyo kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ili zitumike ipasavyo kujenga na kuboresha miundombinu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.
Ndg. Afadhal ameyasema hayo alipotembelea Wilaya ya Sikonge akikagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kupitia miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inawajali wananchi wake kwa kuwasogezea huduma bora za jamii,ikiwemo Afya,Elimu,barabara,maji na miradi mingine mingi ambayo wananchi wananufaika na wataendelea kunufaika nayo.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, kaimu Mganga Mkuu (W) Dkt.Songolo amesema Serikali imetoa Tsh Bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa majengo 10 ya hospitali hiyo huku Halmashauri ikichangia zaidi ya Tsh.Milioni 100 huku akiongeza kuwa mpaka sasa ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 95%.Aidha,Dkt.Songolo ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa kuwapatia fedha hizo na kuongeza kuwa ujenzi wa Hospitali hiyo utasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa, Kupanua wigo wa utoaji huduma sambamba na kupunguza msongamano wa wagonjwa wa nje(OPD) na wagonjwa wanaolazwa katika hospitali teule ya Wilaya(CDH) pamoja na kituo cha Afya Mazinge.
Katika ziara hiyo Ndg.Afadhal ameambata na viongozi mbambali wa Chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya Mkoa na Wilaya akiwemo mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora,M/kiti wa CCM(W),Mhe.Mbunge jimbo la Sikonge,Waheshimiwa madiwani, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji(W) na Wakuu wa Idara mbalimbali wa Halmashauri hiyo.
Na Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa