DIWANI KATA YA SIKONGE AHAMASISHA KUJITOLEA KATIKA MIRADI
Haya yamefanyika leo tarehe 3 Novemba, 2021 katika shule ya Sekondari Ngulu iliyopo Kata ya Sikonge Wilayani Sikonge. Shule hii imepata fedha Milioni 80 Kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa 4.
Akiongoza majitoleo ya uchimbaji msingi wa ujenzi wa madarasa manne, Mhe. Peter Nzalalila ambaye ni Diwani Kata Sikonge na Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge amefurahishwa sana na wingi wa watu waliojitokeza katika zoezi hilo la kuunga mkono juhudi za Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambae ametupatia fedha za mpango wa Miradi ya Maendeleo na mapambano ya UVIKO-19 zaidi ya Bilioni 2 Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Wananchi, Watumishi pamoja na Viongozci wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Anna Chambala wameshiriki zoezi hilo ambalo litasaidia kuokoa fedha ambayo ilipangwa kukamilisha ujenzi wa msingi.
Aidha, Mhe. Nzalalila alimkaribisha mgeni rasmi Mhe. Anna Chambala kusema neno baada ya zoezi la uchimbaji msingi wa madarasa. Mwenyekiti aliwashukuru wote waliojitokeza Kwa niaba ya CCM Wilaya na kusema kuwa hii inaunga mkono Kwa Serikali ya Awamu ya 6 Kwa kutupatia fedha hizi za miradi.
Pia aliwataka Wananchi kujitokeza Kwa wingi pindi wanapotangaziwa shughuli za Maendeleo kama hizo za miradi ili kushiriki kwa wingi.Mhe. Nzalalila maarufu kama BABABABA alihitimisha Kwa kutoa tangazo la kuendelea na kazi hiyo kesho Kwa kuwa mvua ilikatisha zoezi la Leo na kuwaomba wajitokeze Kwa wingi zaidi kesho.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa