DC PALINGO AKUTANA NA WAVUVI MTO KOGA.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo ametembelea MTO Koga kuzungumza na wavuvi na kutatua mgogoro uliokuwepo kati ya wavuvi na mwekezaji wa kitalu cha uwindishaji cha "AFRICAB ADVENTURE".
Akizungumza na wavuvi katika Mto Koga DC Palingo amewataka kufuata sheria na taratibu za uvuvi katika mto huo ambao pia unapita katika hifadhi za misitu na kwamba linasimamiwa na mwekezaji ambae pia anahifadhi na kulinda eneo hilo kisheria.
Aidha,Mhe.Palingo amewataka wavuvi kuwa na vibali halali vya uvuvi na vitambulisho vya uraia ili kubaini wahalifu wanaojificha katika maeneo hayo huku akiwataka wavuvi hao kutoa taarifa endapo kuna watu wasio na sifa za kufanya shughuli za uvuvi.
Kwa upande wake,Meneja wa TFS Catherine Mbwambo amewaasa wavuvi kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu katika hifadhi ikiwemo kukata miti na kutupa taka.
Nao wananchi wanaojishughulisha na Uvuvi Mto Koga wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwatembelea na kutatua Mgogoro kati yao na Mwekezaji. Mkuu wa Wilaya aliambatana na Kaimu Mkurugenzi,Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na Viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa