DC PALINGO AKAGUA MAENDELEO UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA -UVIKO19.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa katika shule za sekondari Mibono,Langwa na Usunga.Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imepokea Tsh.Bilioni 2.77 kupitia mpango wa maendeleo ya ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 Kwa ajili ya kutekeleza miradi mipya, ambapo kati ya fedha hizo Tsh.Bilioni 1.18 zimeelekezwa kujenga vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari kufikia Desemba 15 madarasa hayo yakamilike.
DC Palingo amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kuzingatia maelekezo huku akiwaasa kuacha kuchelewesha ujenzi wa madarasa hayo kwa kuwa tayari serikali ya awamu ya sita imetoa fedha kwa ajili ya madarasa hayo.Kwa upande wao wakazi wa Wilaya ya Sikonge wameipongeza Serikali kwa kuleta fedha hizo kwani zitasaidia kumaliza tatizo la upungufu wa madarasa uliokuwepo hivyo kuongeza kiwango cha wanafunzi wengi kupata elimu bora katika miondombinu bora.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa