DC PALINGO AENDELEA KUHAMASISHA CHANJO YA UVIKO-19.Kiloleli.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo ameendelea kuhamasisha wananchi kuchanja ili kujikinga na ugonjwa hatari wa UVIKO-19 na kuwataka wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo.
Mhe.Palingo ameyasema hayo alipohudhuria Fainali ya mashindano ya mpira wa miguu maarufu kwa jina la "RWAMBANO CUP" yaliyofanyika katika Kata ya Kiloleli.
Akitoa elimu juu ya Chanjo hiyo Kaimu Mganga Mkuu Dkt.Theopister Elisa amesema chanjo ya UVIKO-19 ni salama na imethibitishwa na wataalamu wa tiba kutoka Tanzania,na kuongeza kuwa Mtu anapochanjwa anaepuka kuwa katika hatari ya kifo pale anapopata ugonjwa huo tofauti na mtu ambae hajachanja.
Aidha,Wananchi mbalimbali wamejitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 huku Diwani Viti maalumu kata ya Kitunda Mhe.Ester Kayombi akionesha mfano kwa kuwa wa kwanza kuchanja.
#ujanja ni kuchanja.
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa