CHANJO NI HIARI,NI SALAMA NA NI MUHIMU.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo ameendelea na ziara katika Kata ya Pangale kuhamasisha umuhimu wa Chanjo ya UVIKO-19 akiambatana na wataalamu wa Afya.Mhe.Palingo amewaasa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 ikiwemo kuchanja na kusisitiza kuwa chanjo ni salama.Baadhi ya wananchi wameomba elimu itolewe hasa vijijini ambako bado hawana ufahamu juu ya Chanjo ya UVIKO-19."Naomba wataalamu wa afya wafike maeneo ya vijijini kama Igalula wasiishie mjini mjini tu ili na huko chanjo ziwafikie" Sebastian Mkopi mwananchi kata ya Pangale akitoa maoni baada ya Elimu ya chanjo kutolewa.Kwa upande wake Afisa Afya(W) Laurent Lushekya amesema wameandaa mpango wa kufika maeneo yote ya Wilaya ya Sikonge kwa kutumia njia ya huduma mkoba(Community outreach) ambapo watawafikia wananchi walio maeneo ya Vijijini.Baadhi ya wananchi kata ya Pangale wamejitokeza kupata Chanjo ya UVIKO-19 ikiwa ni njia bora ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.#ujanja ni kuchanja.
Kwa maeezo zaidi bofya link
https://web.facebook.com/100024087722562/videos/pcb.1039551990191049/2985197135061456
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa