Katibu Tawala wa Wilaya ya Sikonge Andrea Ng’hwani amefungua mafunzo ya stadi za maisha kwa Maafisa Elimu kata,walimu wakuu,walimu wa malezi na unasihi,mafunzo hayo yameendeshwa na shirika lisilokuwa la kiserikali CAMFED (Campaign for Female Education) katika ukumbi wa shule ya sekondari Kamagi.
Akifungua mafunzo hayo Ndugu Ng’hwani amewaomba CAMFED kutoa elimu bora kwa walimu watakao simamia mradi huo na kuhakikisha vijana wanapata ujuzi mkubwa na kuelewa kuwa stadi za maisha sio elimu ya darasani bali ni maandalizi ya maisha ya badae kwa vijana kwa kuzingatia malengo na mipango ya serikali kupitia Wizara ya Elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
“Niwasihi kutoa ushirikiano wenu wa dhati kwa pamoja ili kuleta mabadiliko chanya katika elimu na maisha ya vijana watakao jitolea kutekeleza mradi huu kwa kupatiwa nafasi na fursa mbalimbali zinazopatikana katika maeneo ya wilaya kwa kupata motisha ya kazi watakazozifanya ili kufikia malengo yaliyokusudiwa”. Amesema ndugu Ng’hwani.
CAMFED inatarajia kuendesha mafunzo hayo kwa siku mbili ambapo lengo ni kuwajengea uwezo vijana wakuweza kujitolea kusimamia na kuelimisha jamii juu ya maadili na kuepuka mambo yasiyofaa yanayoathiri maadili mema ya nchi yetu.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa