Baraza la maalum la waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Sikonge,likiongozwa na Mhe. Rashid Magope,Mwenyekiti wa Halmashauri, limepokea na kuridhia taarifa ya hesabu za halmashauri kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akiwasilisha taarifa hiyo Kaimu Mweka Hazina Wilaya ya Sikonge Bw. Emmanuel Kihahi amesema ukusanyaji mapato umeongezeka kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ukilinganisha na makusanyo ya mwaka wa fedha uliopita 2021/2022.
Aidha kwa upande wa madeni ya Halmashauri yamepungua toka bilioni 1.2 hadi milioni 748,712,137.Hii imetokana na halmashauri kulipa madeni ya watumishi na watoa huduma mbalimbali.
Akichangia hoja Mhe. Peter Nzalalila Diwani wa kata ya Sikonge amesema ameiomba Halmashauri kufanya utaratibu rafiki kwa mafundi wazalendo(local fundi) ili wakatwe service levy moja kwa moja toka kwenye madai yao kuliko kulipa papo kwa papo kwani wakati wanafuatilia madai yao huwa wanakuwa hawana chochote.
Akijibu hoja hiyo Kaimu Mkurugenzi mtendaji Bwana Nico Kayange amesema “Service levy ni chanzo cha mapato ya serikali ,tunachoweza kufanya nikuwaelimisha wadau wetu ili waweze kuendana na matakwa ya serikali”.
Akifunga kikao hicho cha baraza maalum la madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Sikonge Mhe. Rashid Magope amewataka Wataalam kuepuka kuwa na bakaa kwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya halmashauri ili pia kufanya vizuri kama wengine wanavyofanya vema.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa