Akifungua baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope amesema tumbaku ni zao muhimu la kiuchumi lakini linachangamoto zake za uharibifu wa mazingira hivyo mpango wa urasimishaji misitu ya asili ni muhimu sana kwani utaleta tija kwa mustakabali wa uchumi na mazingira.
Akiwasilisha mpango wa urasimishaji wa misitu ya asili toka Mkwawa Leaf Tobacco Ltd, Bw. Zacharia Joseph Mseswa amesema kumekuwa na nguvu kubwa katika kuteketeza uoto wa asili lakini sio kuokoa au kuhifadhi uoto huo.Ndio maana Kampuni ya Mkwawa imekuja na Mpango mkakati wa kuhifadhi mazingira ya misitu ya asili.
Aidha Waheshimiwa madiwani wakichangia mpango huu wameshauri uwepo uelewa wa mipaka halisi ya maeneo yatakayonufaika na mpango huu kwa kupitia tena majina ya mipaka husika ilikuondoa utata wa mwingiliano wa mipaka katika kata zao.
Akifunga kikao hicho Mhe. Magope amewashukuru sana Waheshimiwa madiwani kwa kubariki mpango huo pamoja na marekebisho yake.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa